Tetesi za soka Ulaya Septemba 16 (Lewandowski, Fernandes, Rudiger, Kounde, Wilshere)

HomeMichezo

Tetesi za soka Ulaya Septemba 16 (Lewandowski, Fernandes, Rudiger, Kounde, Wilshere)

Liverpool imejitokeza kama mojawapo ya klabu ambazo zinamnyatia mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33 anatarajiwa kuondoka Bayern Munich msimu ujao. (Fichajes, Spanish)

Manchester United wamefikia pazuri katika mazungumzo yao na kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes tangu mwezi Julai. Mchezaji huyo (27) anataka kusalia Old Trafford na kandarasi yake inachukuliwa na umuhimu mkubwa pamoja na kiungo wa kati Paul Pogba, 28. (Fabrizio Romano via Twitter)

Beki wa Chelsea Antonio Rudiger huenda akauzwa ili kurahisisha ununuzi wa beki wa Sevilla Jules Kounde. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ujerumani ananyatiwa na klabu za PSG na Real Madrid, lakini ameonekana kuwa kiungo muhimu wa safu ya ulinzi wa mkufunzi Thomas Tuchel. (Football 365)

Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez ameripotiwa kukaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo ya Serie A, ikimaanisha kwamba Arsenal, na Tottenham watalazimika kutumia kitita kikubwa cha fedha iwapo wataamua kuimarisha hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport, Italia)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere hataki makubaliano ya kulipwa kwa mechi atakazoshiriki katika uwanja wa Emirates baada ya mkufunzi Mikel Arteta kumruhusu kushiriki mazoezi katika uwanja wa timu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameichezea England mara 34 lakini amekosa klabu tangu alipoondoka Bournemouth mapema mwaka huu. (Metro)

error: Content is protected !!