Leo katika historia

HomeElimu

Leo katika historia

Mwaka 1810: Chile ilipata uhuru wake kutoka Hispania iliyoitawala nchi hiyo tangu karne ya 16. Chile ina eneo la kilomita za mraba 4,300 katika mwambao wa Bahari ya Pasifiki na mji mkuu wake unaitwa Santiago.

Mwaka 1502: Christopher Columbus alifika katika eneo la Costa Rica katika safari yake ya nne na ya mwisho. Columbus ndiye aliyegundua Bara la Amerika.

Mwaka 1962: Rwanda, Burundi, Jamaica na Trinidad ziliandikishwa kuwa wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN). UN ilianzishwa mwaka 1945 ili kuwa kiungo kati ya mataifa yote ulimwenguni na kulinda amani.

Mwaka 1906: Kimbunga kikali cha Tsunami kiliua watu 10,000 katika Mji wa Hong Kong nchini China. Tsunami na tetemeko la ardhi liliikumba pia Japan mwaka 2011 na kusababisha madhara makubwa.

error: Content is protected !!