Youtube yafuta nyimbo 4 za Otile Brown

HomeKimataifa

Youtube yafuta nyimbo 4 za Otile Brown

Jacob Odunga, maarufu kama Otilie Brown msanii kutoka Kenya amelalamika baada ya kufutwa kwa nyimbo zake 4 zenye watazamaji zaidi ya milioni 10 kwenye mtandao wa Youtube.

Otilie ametoa malalamiko hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba amejisikia vibaya sana baada ya kugundua hilo kwani sio jambo dogo kwa msanii kutoka Kenya kufikisha watazamaji wengi hivyo.

Aidha amewajibu mashabiki wanaosema kwamba kufutwa kwa video hizo ni kiki akiandika “what don’t y’all get. Some “people” are deleting our videos/songs on YouTube, is everything kiki to y’all ?? ameandika hivyo kwenye ukurusa wake wa Instagram kwamba yeye hausiki na kufutwa kwa video hiyo nasio kiki.

Nyimbo zilizofutwa ni Such Kind of Love, Duduma, Chaguo la moyo na Aiyana ambazo ni kati ya ngoma zilizopokelewa vyema na mashabiki na kuendelea kufanya vizuri mpaka sasa.

error: Content is protected !!