Serikali yasitisha mfumo mpya wa ukusanyaji ada za maegesho

HomeKitaifa

Serikali yasitisha mfumo mpya wa ukusanyaji ada za maegesho

Kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu changamoto zinazojitokeza wakati wa ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu amesitisha kwa muda matumizi ya mfumo huo kuanzia leo tarehe 09.10.2021.

Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kukutana na timu va Wataalamu wa TARURA kujadili namna ya kutatua
changamoto zilizojitokeza.

    > Mfumo mpya wa maegesho Dar, fahamu jinsi ya kulipia, faida na changamoto zake

Aidha, wakati hayo yakiendelea ameagiza ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari zitaendelea kukusanywa kwa kutumia mfumo wa awali(Manual system) ambao ulikua unatumika kukusanyia ada hiyo kabla ya kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki (TeRMIS).

Mfumo wa Kieleketroniki wa ukusanyaji wa ada za maegesho ulianza kutumika katika mkoa hivi karibuni lengo ikiwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa chanzo hicho na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

error: Content is protected !!