KFC Kenya kuanza kuuza ugali baada ya kuishiwa viazi vya ‘chipsi’

HomeKimataifa

KFC Kenya kuanza kuuza ugali baada ya kuishiwa viazi vya ‘chipsi’

Mwanzoni mwa mwaka 2022 KFC Kenya ilipata changamoto ya kuishiwa kwa viazi wanavyotumia kuandaa ‘chipsi’ na kufanya wengi kujiuliza kwanini wanashindwa kununua viazi kutoka kwa wakulima wa ndani kwani vipo vya kutosha, lakini Mkurugenzi Mkuu wa KFC Afrika Mashariki Jacques Theunissen ameeleza sababu kubwa inayowafanya wasichukue hatua ya kununua viazi kutoka kwa wakulima.

“Sababu ambayo hatuwezi kununua bidhaa za ndani kwa sasa ni kwamba wasambazaji wote wanahitaji kupitia mchakato wa kiidhinisho wa QA wa kimataifa na hatuwezi kukwepa hilo hata kama tutaishiwa ili kuhakikisha kuwa chakula chetu ni salama kwa matumizi ya wateja wetu. KFC Kenya kuanza kuuza ugali baada ya kuishiwa viazi vya ‘chipsi” alisema Jacques Theunissen.

Lakini kupitia mtandao wa Instagram wa KFC Kenya wameandika kwamba kuna chakula mbadala ambacho ni ugali ambapo mteja anaweza kuchagua badala ya ‘chipsi’ kama ilivyozoeleka na wengi.

“Mlikula siku ya  sherehe na starehe na vipendwa vyako vyote vya KFc. Kwa sasa Chipsi tumeishiwa. samahani! timu yetu inafanya kazi kwa bidii kutatua suala hilo. kwa sasa tumependekeza baadhi ya chaguzi za kubadilishana kwa milo kama ugali ikiwa unatamani kuku wetu,” limeandika chapisho hilo.

error: Content is protected !!