Waumini wamkataa Mchungaji aliyeiba Mke wa Mzee wa Kanisa

HomeKitaifa

Waumini wamkataa Mchungaji aliyeiba Mke wa Mzee wa Kanisa

Mchungaji wa Ushirika mmoja wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri mkoani Morogoro analalamikiwa kwa tuhuma za kuchukua mke wa aliyekuwa Mzee wa Kanisa hilo mwanzoni mwa miaka ya 2000  kabla ya kuhama kanisa.

Waumini wa Kanisa hilo wameeleza kuwa kinachowasikitisha ni kitendo cha mchungaji huyo kurejea katika Kanisa hilo akiwa na mkewe (ambaye alikuwa Mke wa Mzee wa Kanisa)  na kupewa Uchungaji katika Kanisa hilo.

Muumini mmoja alisema ” Tulishtushwa sana kusikia tumepangiwa kutunzwa kiroho na Mchungaji aliyevunja ndoa ya aliyekuwa Mzee wa Kanisa lake. Huyu ataawashauri nini wanandoa? hii ni aibu kwa kanisa”.

Waumini katika kanisa hilo wameomba uongozi wa juu unaosimamia  makanisa hayo kushughulikia tatizo hilo kwani wamesema haiwezekani “mke” wa Mchungaji kuitwa “Mama Mchungaji” na kuwaongoza kiroho. #clickhabari

error: Content is protected !!