Ajinyonga kwa kamba za viatu

HomeKitaifa

Ajinyonga kwa kamba za viatu

Mwanaume mmoja mkazi wa Mtaa wa Rungwa kata ya Kazima Manispaa ya Mpanda, Edmond Sungura (53) amekutwa amejinyonga hadi kufa chumbani kwake kwa kutumia kamba za viatu vyake.

Taarifa ya kifo chake imeripotiwa na mke wa marehemu Astilida Mkambila ambaye amesema kwamba aligundua tukio hilo Januari 2, asubuhi baada ya kumuamsha pasipo mafanikio na kueleza kwamba marehemu alirudi nyumbani akiwa amelewa pombe na alimuita chumbani kisha kumkabidhi simu mbili.

“Aliniambia chukua simu ziweke mezani, hii moja ni ya rafiki yangu nimeona amechoka sana atakuja kuichukua asubuhi, nikazichukua nikaenda sebuleni kuangalia TV na watoto,”

“Akatoka chumbani akasema naomba muondoke mtoke nje, akazima TV tukatoka, akatufata akasema hapa ndiyo nje? Naomba mtoke nitawachafua,” alisema Astilida.

Astilida pia akaendelea kueleza kwamba asubuhi waliamka akaanza kumuita mme wake lakini hakupata jibu na ndio alipoaamua kuchukua uamuzi wakuchana wavu wa dirisha na kumuona ameninginia kwenye paa la nyumba

error: Content is protected !!