Mfahamu Mchungaji wa kwanza mwanamke toka jamii ya Kimasai

HomeKitaifa

Mfahamu Mchungaji wa kwanza mwanamke toka jamii ya Kimasai

Mchungaji Rebecca Maduley Kurubai, anaingia katika rekodi kuwa Mwanamke kutoka kabila la kimasai Tanzania kupadrishwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (ELCT) Dayosisi ya Kusini.

Mchungaji Kurubai amekuwa akiendesha mafundisho katika jamii inayomzunguka na anaeleza kuwa mafundisho yake yamevuta watu wengi sana kanisani.

Kwa sasa yuko mkoani Njombe katika Seminari ya Kidugala ambapo anafanya utafiti wa shahada yake ya uzamivu.

Kurubai anasema alimaliza masomo yake mnamo mwaka 1999 ana akafanikiwa kusimikwa kuwa mchungaji mwaka huohuo na kuhamishiwa Mkoani Iringa kutoa huduma ya kiroho.

Alipofika Iringa ilimuwia vigumu kuanza kazi hiyo kwani hakuwa na nyenzo kama ofisi, wala sehemu ya kuendeshea ibada ingawa baada ya muda walijitokeza watu wenye nia ya kumsaidia kuanzisha kanisa dogo na taratibu alianza kupata waumini ingawa wengi walikuwa wakishangaa inakuwaje “Mmaasai” amekuwa mchungaji wakati wengi wamezoea kuona wamasai wakiishi maisha ya tofauti.

Kwa sasa Kanisa lake lina waumini wengi sana licha ya kuwa na changamoto ndogondogo, lakini pia anaamini iko siku pia ataweza kufikisha neno la Mungu kwa ukubwa zaidi na kumfikia kila mtu, ikiwamo jamii yake ya kabila la kimasai.

error: Content is protected !!