Fahamu sababu za wabunge 19 wa CHADEMA kubaki bungeni

HomeKitaifa

Fahamu sababu za wabunge 19 wa CHADEMA kubaki bungeni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, ameweka wazi kwamba wanachama 19 waliopo bungeni kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni halali kwakueleza kwamba ili mbunge asiwe na uhalali wa kuwa bungeni basi lazima chama kipeleke taarifa mahususi kwenye bunge yakumfuta uanachama mbunge huyo.

“Kwanza uharamu haupo kwa sababu huwezi kuwa haramu alafu akawa mule ndani, lakini nataka nifafanue jambo moja, nchi yetu ninyi mnafahamu na mimi nina fahamu inaendeshwa kidemokrasia lakini kisheria jambo moja tu ambalo linasubiriwa ni watu kumalisha michato yao,”

“Mbunge lazima awe mwanachama wa chama fulani kwahiyo mtu akifukuzwa uanachama na chama fulani anakuwa hana uhalali wakuwepo bungeni lakini kwa sababu ya demokrasia ile michakato lazima iwe imemalizwa bunge liletewe taarifa mahususi kwamba mtu huyi sio mwanachama wa chama fulania naondoka,” Spika Tulia.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA ni HaIima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

 

error: Content is protected !!