Afukuliwa siku moja baada ya kuzikwa

HomeKitaifa

Afukuliwa siku moja baada ya kuzikwa

Mwili wa marehemu, Mark Mkude mwenye umri wa miaka 67 umefufuliwa baada ya kuzikwa na na ndugu wa marehemu mwingine, Gervas Chondoma mwenye umri wa miaka 71 huku taarifa zikisema kwamba wote walifariki Februari 9, mwaka huu na miili yao ilikuwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Mdogo wa marehemu Gervas Chondoma, Mohamed Mkwama alisema kuwa mwili wa kaka yake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro ambapo Februari 10 watoto wa marehemu pamoja na ndugu wachache walikwenda kuchukua mwili huo kwa ajili ya mazishi.

Mkwama alisema alishtuka sana baada ya kupigiwa simu na baadhi ya ndugu na kumueleza kuwa mwili waliouzika haukuwa wa ndugu yao na kwamba mwili wa ndugu yao waliuacha katika chumba cha kuhifadhia maiti.

“Nilipofika makaburini nilikuta ndugu wa marehemu tuliyemzika wakisubiri tufukue kaburi ili wachukue mwili wa ndugu yao na ilibidi tufanye hivyo,” alisema Mkwama.

 

error: Content is protected !!