Mke wa Ndugai avunja ukimya juu ya alipo mumewe

HomeKitaifa

Mke wa Ndugai avunja ukimya juu ya alipo mumewe

Fatuma Mganga mke wa aliyekuwa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kuwa mumewe wake yuko salama kabisa ila kwa sasa ameamua kuishi maisha yake ya kawaida kama wananchi wengine hataki tena kujihusisha na umma hivyo mumewe aachwe aishi maisha yake binafsi.

Fatma Maganga ambaye ni katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma, anasema hakuna ulazima wa watu kujua wapi mumewe aliko na kama kuna watu wanataka kujua wapi aliko wampigie mwenyewe Ndugai.

“Mkiona mke wake yuko kazini jamani, si mnajua yuko salama, angekua hayuko vizuri mngeniona kazini? Ningekuwa namhudumia, lakini yuko vizuri anaendelea na maisha yake sasa ni mwananchi kama wananchi mwingine” alisema Fatma.

Job Ndugai tangu alijiuzulu nafasi yake ya spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 6, hakuwahi kuonekana katika shughuli zozote za chama wala za kiserikali. Pamoja na kwamba vikao vya bunge vimeanza na yeye ni mbunge wa jimbo la Kongwa lakini hakuwahi kuonekana pia kwenye vikao vya bunge.

Viongozi mbalimbali waliulizwa ili kujua ni wapi Ndugai alipo au kama aliwahi kuonekana au kutoa taarifa yote lakini juhudi hizo zilishindikana kutokana na viongozi hao kushindwa kutoa ushirikiano. Miongoni mwa viongozi hao ni Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi na Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa Joyce Nkaugala.

error: Content is protected !!