Watanzania 33,000 hufariki kila mwaka sababu ya moshi wa kupikia

HomeKitaifa

Watanzania 33,000 hufariki kila mwaka sababu ya moshi wa kupikia

Wastani wa Watanzania 33,000 hufariki kila mwaka, kutokana na moshi wa kupikia.

Waziri wa Nishati January Makamba alisema hayo jana jijini Dodoma, wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Wabunge wanawake kuhusu matumizi ya nishati mbadala nyumbani.

Makamba ambaye yuko nje ya nchi kikazi, alitoa ujumbe huo ambao ulirekodiwa kabla ya kusafiri.

“Nilitamani kuhudhuria semina hii, lakini nimepata safari niko nje ya nchi, lakini kabla sijaondoka nilisema nitaacha rekodi ya ujumbe wangu,” alisema.

Alisema kuwa wastani wa Watanzania 33,000 wanakufa kila mwaka, kutokana na moshi wa kupikia kwa kuugua magonjwa ya mfumo wa hewa.

Alisema matumizi ya nishati mbadala yataokoa maisha ya kinamama na wote wanaotumia kuni.

“Saa moja kwenye jiko lenye moshi ni sawa na kuvuta sigara 300, ukimpima mwanamke wa Kijijini kwa X-ray ni kama mtu aliyevuta sigara muda mrefu, ule moshi ambao ni sumu unaofanya hata wadudu wasikae jikoni ndio unaingia kwenye mapafu,” alisema.

Alisema kuwa hiyo inonesha wanawake Tanzania wanameza moshi unaowaua taratibu.

” Madhara mengine ni watoto kuzaliwa njiti na mimba zinazotoka, ule moshi wa kupikia madhara yake hayazunguzwi sana, tunatakiwa kuchukua hatua. zinazostahili katika kumkomboa na kumsaidia mwanamke,” alisema.

error: Content is protected !!