Rais Samia: Viongozi simameni imara

HomeKitaifa

Rais Samia: Viongozi simameni imara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasihi viongozi wa mkoa wa Singida kuhakikisha wanasimama imara katika utekelezaji wa majuku yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia tarehe 16 Oktoba, 2023

Amesema hayo leo tarehe 10 Oktoba, 2023 wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Bombadia ambapo leo mkoa wa Singida unaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

“Niombe viongozi wa mkoa, wilaya na kata za mkoa muende mkasimame imara simamieni kazi zenu, hudumie wananchi ambayo ndio kazi kubwa tumeletewa huku Singida.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewahakikisha wananchi wa mkoa wa Singida maendeleo endelevu na kwamba Serikali yake imejidhatiti katika kuboresha mazingira bora ya kuwezesha shughuli za uwekezaji.

“Kwa upande wetu Serikali Kuu tutaendelea kuunga mkono jitihada za vipaumbele vya maendeleo vya mkoa wa Singida kwa kuhakikisha tunajenga mazingira wezeshi.” amesema Rais Samia

 

 

 

error: Content is protected !!