Viongozi hakuna kutoka mpaka sensa imalizike

HomeKitaifa

Viongozi hakuna kutoka mpaka sensa imalizike

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amewaagiza viongozi wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya kubaki katika vituo vyao vya kazi hadi shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi itakapokamilika.

Viongozi hao ni pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tawala wa mikoa na wilaya.

“Kutokana na umuhimu huu, nina elekeza wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi kuendelea kuwa katika maeneo ya kazi mpaka zoezi la sensa litakapo kamilika.” amesema Waziri Bashungwa.

Amesema iwapo itatokea dharura ambayo italazimisha watumishi hao kutoka kwenye maeneo yao ya kazi lazima watoe taarifa ya dharura hiyo.

 

error: Content is protected !!