Agizo la Rais Samia baada ya kutembelea mradi wa maji Arusha

HomeKitaifa

Agizo la Rais Samia baada ya kutembelea mradi wa maji Arusha

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 15, 2021 ametembelea mradi wa maji wa bilioni 520 unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) na kuagiza mradi huo kukamilika kwa wakati.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Chekereni wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Rais Samia amesema mradi huo unakwenda kumaliza tatizo la maji kwa wakazi wa jiji la Arusha. Pia amesisitiza mradi huo unapaswa kuwagusa wananchi ambao wanapitiwa na bomba la mradi huo.

  > Rais Samia kufanikisha ujenzi wa jengo la tiba ya mionzi KCMC

Amesema kufikia mwezi Juni mwakani wananchi wote wa Arusha watakuwa wakipata majisafi na salama yasiyo na chumvi.

Naye Waziri wa Maji, Juma Awesso akizungumzia mradi huo, amesema ni mkubwa na kwamba utatoa maji lita milioni 200, wakati mahitaji ya maji ya jiji la Arusha ni lita milioni 109 tu.

“Kwa sasa asilimia 65 ya wananchi wa Arusha tayari wameanza kupata maji,” amesema aweso.

Waziri Awesso amewatoa hofu wananchi wa vijiji ambavyo mradi huo unapita kuwa wote watapatiwa huduma hiyo.

error: Content is protected !!