Rais Samia afungua milango ya uwekezaji

HomeKitaifa

Rais Samia afungua milango ya uwekezaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaalika wawekezaji wa Dubai kuja kuwekeza nchi huku akiwahakikishia mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya biashara.

Rais Samia amesema hayo alipokua akihutubia katika mkutano ulioshirikisha wawekezaji, wafanya biashara, Mwanamfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na viongozi wengine waliohudhuria Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ( Dubai Expo) yanayoendelea nchini humo.

“Nipende kuchukua fursa hii kuwakaribisha nyote nchini Tanzania kwani kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya biashara,”

“Njooeni wote Tanzania, Tanzania inawasubira na kama kuna mtu anawaza kufanya biashara na uwekezaji basi fikiria Tanzania,” alisema Rais Samia Suluhu. 

 

error: Content is protected !!