Simu 50 zitakazofungiwa kabisa kutumia WhatsApp kuanzia Novemba 1, 2021

HomeKimataifa

Simu 50 zitakazofungiwa kabisa kutumia WhatsApp kuanzia Novemba 1, 2021

Kama wewe ni mtumiaji wa WhatsApp, basi unapaswa kukaa chonjo sana na utazame simu yake kama imo kwenye idadi ya simu ambazo zitashindwa kabisa kutumia mtandao huo ifikapo mwezi Novemba  2021.

Gazeti la mtandaoni la nchini Uingereza, The Sun, limeripoti kwamba aina 50 za simu zitashindwa kabisa kupakua mtandao WhatsApp, hivyo watu watalazimika kununua simu mpya endapo watataka kutumia mtandao huo. Mchakato wa kuzima WhatsApp kwenye zaidi ya aina ya simu 50 utaanza Novemba 1 mwaka huu.

Kwa wale wanaotumia mfumo wezeshi wa Android, watapaswa kuboresha mifumo yao hadi Android 4.1 au zaidi ya hapo, lakini hii bado inaweza isisaidie sana kama utakuwa mtumiaji wa aina ya simu zilizotajwa. Kwa wale wa iPhone, basi angalau awe na mfumo tumishi wa iOS 10.

Simu kama Samsung Galaxy S3 na Huawei Ascend Mate, zitakosa kabisa huduma ya WhatsApp, hawa watafute simu nyingine tu. Wanaotumia iPhone 4S, watashindwa pia kutumia WhatsApp, kwa sababu mfumo wa iOS 10 hauwezi kukaa ndani ya iPhone 4S.

Kama ni mtumiaji wa iPhone 6S, iPhone 6S Plus, iPhone SE, iPhone 5 na aina nyingine zote za iPhone 6, zitapaswa kuboreshwa kwenda mfumo wa iOS 10 ili kuendelea kutumia WhatsApp.

Apple na Google huwa na utaratibu wa mara kwa mara kufanya huduma zao kutopatikana kwenye simu ambazo zimepitwa na wakati, kwa kuwa ni gharama zaidi kwenye uendeshaji wa programu zao kwenye simu za zamani, pia sio salama hasa kwenye ulinzi dhidi ya udukuzi, hivyo ni lazima wazuie baadhi ya simu kwa usalama wa watumiaji.

> Zijue aina za habari ambazo huruhusiwi kuweka Facebook sasa

> Wanaotumia iPhone hizi, hatarini kuikosa WhatsApp

Simu 50 ambazo zitaikosa WhatsApp kuanzia Novemba 1, vipi simu yako iko salama?

1. Galaxy Trend Lite
2. Galaxy Trend II
3. Galaxy SII
4. Galaxy S3 mini
5. Galaxy Xcover 2
6. Galaxy Core
7. Galaxy Ace 2
8. Lucid 2
9. Optimus F7
10. Optimus F5
11. Optimus L3 II Dual
12. Optimus F5
13. Optimus L5
14. Best L5 II
15. Optimus L5 Dual
16. Best L3 II
17. Optimus L7
18. Optimus L7 II Dual
19. Best L7 II
20. Optimus F6, Enact
21. Optimus L4 II Dual
22. Optimus F3
23. Best L4 II
24. Best L2 II
25. Optimus Nitro HD
26. Optimus 4X HD
27. Optimus F3Q
28. ZTE V956
29. Grand X Quad V987
30. Grand Memo
31. Xperia Miro
32. Xperia Neo L
33. Xperia Arc S
34. Alcatel
35. Ascend G740
36. Ascend Mate
37. Ascend D Quad XL
38. Ascend D1 Quad XL
39. Ascend P1 S
40. Ascend D2
41. Archos 53 Platinum
42. HTC Desire 500
43. Caterpillar Cat B15
44. Wiko Cink Five
45. Wiko Darknight
46. Lenovo A820
47. UMi X2
48. iPhone 6S Plu
49. iPhone 6S
50. iPhone SE

error: Content is protected !!