Jose Mourinho anukia Newcastle United

HomeMichezo

Jose Mourinho anukia Newcastle United

Stori kubwa kwenye michezo wiki iliyopita ni klabu ya Newcastle United kununuliwa na mabilionea kutoka Saudi Arabia, hatua inayoifanya klabu hiyo kuwa namba moja miongoni mwa wamiliki wenye mkwanja mrefu zaidi.

Kocha anayetambulika kutoishiwa na vibweka, Jose Mourinho ni kocha nambari moja anayehusishwa kwa karibu zaidi kupata kandarasi ya kukinoa kikosi cha Newcastle United chenye maskani yake Kaskazini Mashariki wa England katika mji wa Tyne and Wear.

Mourinho baada ya kuongea na vyombo vya habari amesema kuwa ana mapenzi na klabu hiyo, “Nina mapenzi na hisia na klabu ya Newcastle United”… Alisema. Mourinho amesema hivyo hasa ikizingatiwa kuwa katika miaka ya 90 aliwahi kufanya kazi na moja na nguli wa klabu ya Newcastle, Sir Bobby Robson.

Jose Mourinho amesema kuwa kwa sasa hawezi kuongea zaidi juu ya yeye kujiunga na Newcastle, kwani ndio msimu wake wa kwanza katika klabu ya AS Roma na ana furaha sana kuwa hapo kwa sasa.

error: Content is protected !!