Tetesi za soka Septemba 22 (Martial kuondoka, Guardiola avutwa Barca)

HomeMichezo

Tetesi za soka Septemba 22 (Martial kuondoka, Guardiola avutwa Barca)

Tetesi za Soka Barani Ulaya leo Septemba 22, 2021: Laporta, Bernd Leno, Henderson, Kante, Lewandowski, Oyarzabal, Asensio

Rais wa Barcelona Joan Laporta hajakata tamaa kujaribu kumshawishi bosi wa Manchester City, Pep Guardiola arejee Nou Camp. Guardiola, 50, aliongoza Barca kushinda mataji matatu ya Ligi ya Uhispania na ligi mbili za Mabingwa wakati wa kipindi chake cha miaka minne akiwa kocha kati ya 2008 na 2012 (El Nacional – Spanish).

Arsenal itamfanya kipa wa Ujerumani Bernd Leno, 29, apatikane kwa uhamisho kufuatia kuwasili majira ya kiangazi kwa kipa wa Uingereza 23 Ramsdale (Eurosport).

Mlinda mlango wa Manchester United na England Dean Henderson, 24, anataka uhamisho wa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari (Sun).

Kiungo wa kati wa England wa Huddersfield Lewis O’Brien, 22, amekubali masharti ya mkataba mpya na Terriers licha ya ofa nne kutoka kwa Leeds United ya Ligi Kuu England (Football Insider).

Barcelona inajiandaa kuachana na kocha mkuu Ronald Koeman, huku bosi wa Ubelgiji Roberto Martinez akiwa “chaguo bora” kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo (Goal).

Chelsea inaandaa ofa mpya za mkataba wa kiungo wa England Mason Mount, 22, kiungo wa Ufaransa N’Golo Kante, 30, na kiungo wa Italia 29, Jorginho (Standard).

Chelsea walikuwa tayari kutoa euro milioni 100 (pauni milioni 86) kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain na mlinzi wa Brazil Marquinhos, 27, majira ya joto (RMC Sport – French).

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial atakuwa huru kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 yuko huru kukaa katika Ligi ya England lakini anaweza kutafuta fursa barani, na Barcelona inaweza kuwa chaguo (Eurosport).

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anasema ‘sio lazima ajithibitishe katika ligi nyingine’ baada ya kushinda tuzo la mfungaji bora kwa kufunga mabao 41 Bundesliga na klabu yake ya Bayern Munich msimu wa 2020-21 (Mirror).

Manchester City wanafuatilia fowadi wa Real Sociedad na Uhispania Mikel Oyarzabal, 24 (TeamTalk).

Winga wa Uhispania Marco Asensio, 25, anaweza kuondoka Real Madrid ikiwa hatapewa nafasi zaidi za kikosi cha kwanza chini ya Carlo Ancelotti msimu huu (Cadena Ser – Spanish).

Kiungo wa Ureno Joao Palhinha, 26, yuko tayari kupandishiwa mshahara huko Sporting Lisbon akihusishwa na kuhamia Everton, Tottenham na Wolves msimu huu wa joto (A Bola – Portuguese).

Mlinda mlango wa Ajax na Cameroun Andre Onana, 25, anavutia nia kutoka Inter Milan na Napoli (Calciomercato – Italian).

error: Content is protected !!