Miriam Odemba aanzisha kampeni yakumnunulia gari Wema Sepetu

HomeBurudani

Miriam Odemba aanzisha kampeni yakumnunulia gari Wema Sepetu

Mwanamitindio na mshindi wa taji la Miss Temeke mwaka 1997, Miriam Odemba ameungana na mfanyabiashara Johana Mathysen maarufu kama Director Joan na kuanzisha mchango wakumnunulia gari jipya muigizaji Wema Sepetu nakusema kwamba atake asitake gari atapelekewa.

Miriam ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwakuweka namba za simu ambayo ndio itahusika katika kupokea pesa za mchango kutoka kwa wadau mbalimbali na kuongezea kwamba watu maarufu watoe kuanzia shillingi laki moja ili kuweza kufanikisha jambo hilo.

“Gari litanunuliwa hapa Instagram,Wema atake asitake anapelekewa gari ndio supporters wameniambia…kwa watu wanao fahamika mmesema watoe 100,000 right? Haya Director Joan watanzania wameamua kununua gari kwa ajili ya Tanzanian Last Born,” ameandika Miriam Odemba.

Hili linakuja baada ya mfanyabiashara Aristote kusema kuwa Wema hana gari huku akisema asifananishwe na muigizaji Irene Uwoya jambo ambalo limeibua hisia kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi na watu mashuhuri wakipingana na kauli za Aristote wakidai amefanya unyanyasaji wa mtandaoni.

error: Content is protected !!