Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi kujinyonga kwa askari mahabusu

HomeKitaifa

Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi kujinyonga kwa askari mahabusu

Baada ya kuwepo kwa maneno ya sintofahamu kuhusu tukio la kujinyonga hadi kufa kwa Msaidizi Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Grayson Mahembe, Jeshi hilo la Polisi mkoani Mtwara limetoa ufafanuzi na kueleza namna ambavyo tukio hilo lilitokea na kutaka jamii kupuuza na taarifa za uongo kutoka kwa baadhi ya watu.

Katika taarifa kutoka kwa Jeshi hilo limesema kwamba, baada ya kukamatwa kwa baadhi ya Maafisa, Wakaguzi na ASkari wengine waliohusika na mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi na kisha kuutupa mwili wake vichakani, uchunguzi ulianza kufanyika na kila mtuhumiwa aliwekwa mahabusu la peke yake akiwemo marehemu Grayson.

Taarifa hizo pia zinaeleza baadaye waligundua Grayson amejinyonga na ndipo taratibu za tukio kama hilo zikafuatwa ikiwepo kupiga picha na kuchunguza mwili (postmortem) na daktari akathibitisha kwamba kifo kilitokana na kujinyonga.

Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza namna ambavyo Askari yeyote aliyefariki kwa kujinyonga huwa hazikwi kijeshi, kwa namna kwamba hakuna gwaride la mazishi litakalochezwa na risasi au mabomu yakishindo kupigwa  kwani anahesabiwa kwamba hajafa kishujaa na hastahili heshima hiyo.

error: Content is protected !!