Amuua mtoto na kumtupa Riverside

HomeKitaifa

Amuua mtoto na kumtupa Riverside

Latifa Bakari (33) mkazi wa Mabibo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake mwenye umri wa miaka miwili.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishina Msaidizi (ACP) Jumanne Muliro, alisema jana kuwa Latifa aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Aprili 5 mwaka huu alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga mtoto huyo kupita kiasi na kisha kuutupa mwili katika mto uliopo Ubungo Riverside.

“Baada ya majirani kutomwona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida, walitoa taarifa polisi na alipohojiwa kwa kina mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo na kwenda kuwaonyesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa,” alisema Muliro.

Kamanda Muliro aliongeza kuwa mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

error: Content is protected !!