Romania kufadhili wanafunzi 10 wa Tanzania

HomeKimataifa

Romania kufadhili wanafunzi 10 wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye pamoja na mgeni wake Rais wa Romania, Klaus Iohannis wamekubaliana kutoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa nchi zote mbili.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ikulu Dar es Salaam leo Novemba 17,2023 , Rais Samia amesema lengo ni kuongeza wigo wa ufadhili wa masomo hususani kwenye fani za udaktari na ufamasia.

“Tumezungumzia pia kuhusu kuongeza wigo wa ufadhili wa masomo hususani kwenye fani za udaktari na ufamasia lakini kutokana kwa uhusiano mzuri Romania imekubali kwa mwaka huu kutoa nafasi 10 za masomo kwa watanzania katika maeneo tutakayoyachagua.”

“Tanzania nasi tumetoa nafasi tano za ufadhili kwa vijana wa Romania waje Tanzania katika maeneo na vyuo watakavyovichagua.” amesema Rais Samia Suluhu.

Rais wa Romania yupo nchini kwa ziara ya kitaifa inayolenga kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Romania pamoja na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kama Uwekezaji, Elimu, Utalii, Afya na Utamaduni.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!