Biashara United kibaruani leo nchini Djibouti

HomeMichezo

Biashara United kibaruani leo nchini Djibouti

Timu ya Biashara United leo itashuka dimbani kuvaana na Dikhil FC ya Dijibouti, katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Stade du Ville majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Kwa maelezo ya Katibu wa Biashara United, Haji Mtete amesema wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya FC Dikhil na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi, tutafanya vizuri,” amesema Mtete.

Hii ni mara ya kwanza kwa Biashara United kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.

error: Content is protected !!