Mbowe afikishwa makamani mbele ya jaji mpya

HomeKitaifa

Mbowe afikishwa makamani mbele ya jaji mpya

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa asubuhi na kupelekwa moja kwa moja katika mahabusu ndogo iliyopo katika Mahakama hiyo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Hata hivyo muda mfupi baadaYe, washtakiwa hao wamepelekwa mahakama ya wazi, maalumu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Washtakiwa hao wanatarajia kuendelea kusikiliza kesi yao mbele ya Jaji Mustapher Siyani, baada ya Jaji Elinaza Luvanda kujitoa kusikiliza kesi hiyo siku ya Jumatatu na kupelekea kesi hiyo kusimama kwa siku nne.

Luvanda alijitoa kuisikiliza baada ya washtakiwa kutokuwa na imani naye kwamba hawaamini kama atawatendea haki baada ya kutupilia mbali mapingamizi waliyoweka awali.

error: Content is protected !!