Mambo 5 ya msingi kuzingatia unapotafuta jina la biashara

HomeBiashara

Mambo 5 ya msingi kuzingatia unapotafuta jina la biashara

Jina la biashara ni kitu muhimu na moja ya utambulisho wa kwanza wa bidhaa zako katika soko hivyo ni muhimu kuwa na uhakika na jina unalotaka kutumia katika biashara. Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia kwenye kuchagua jina la biashara yako.

1. Mahitaji ya mtandao
Ufanyaji wa biashara umebadilika sana hasa kutoka na ukweli kwamba teknolojia imetawala sana soko la biashara kutokana na urahisi wake wa kukutanisha wateja na mtoa huduma. Hali hii imepelekewa ongezeko la wafanyabiashara kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na Twitter na pia kuongeza matumizi ya barua pepe na ramani katika mifumo kama google (google maps). Mabadiliko haya yanakulazimu kutafuta na jina la kampuni ambalo halipo na halijwahi kutumika kabla kwenye mitandao la sivyo hautaweza kutumia jina la kampuni yako kwenye mitandao, kitu ambacho kinaweza kuleta mkanganyiko kwa wateja. Mfano biashara ni Kwanza ltd lakini unatumia Mwisho Ltd kwenye mitandao

2. Uhusiano wa jina na huduma au bidhaa
Kutumia jina la biashara ambalo linendana na huduma au biashara yako itasaidia kufikia wateja kwa haraka inapotokea mteja anataka huduma au bidhaa. Hili litasaidia mteja kukumbuka haraka kampuni yako anapotaka huduma husika mfano unauza ‘Juice’ unaweza ukaita ‘Nana Juice’ badala ya Nana pekee. Katika hatua za ukuaji, pale biashara inapokomaa unaweza kufanya maboresho kwa kutenganisha jina la huduma na biashara.

3. Jina fupi na linaloeleweka
Chagua jina fupi na linaloeleweka, na usitumie majina magumu yasioleweka kwani halitazoeleka kwa haraka. Ni ngumu kwa mteja kukumbuka jina gumu.

4. Upekee
Kutumia jina la peke yako lenye upekee litakusaidia kutokuingia kwenye migogoro na kampuni ambazo tayari zipo kwani kila kampuni inakuwa imesajili jina la kampuni na kupata umiliki halali wa jina hilo, hivyo inabidi uwe  na jina lako lenye upekee lisilofanana na majina yaliyopo.

5. Matumizi ya baadaye
Jina la biashara linatakiwa liwe na uwezo wa kuishi muda mrefu. Hii ni kwa sababu mazingira ya ufanyaji biashara yanabadilika kwa uharaka hivyo jina la biashara yako linapaswa kuweza kudumu katika vipindi tofauti.  Mfano endapo utaamua kuipa jina kampuni/biashara kutokana na mwenendo au teknolojia iliopo wakati huo ‘trend’ basi endapo ikitokea hiko kitu kikapotea au kikaisha utalazimika kubadilisha jina na hata kama utaendelea kutumia litakua limepoteza mvuto.

error: Content is protected !!