Mbinu 3 bora za kumkosoa Boss wako

HomeElimu

Mbinu 3 bora za kumkosoa Boss wako

Sio kweli kwamba Boss hakosei kama inavyoaminika. Boss ni binadamu kama binadamu wengine hivyo hayuko kamili na anakosea pia. Kutokana na utofauti uliopo wa kimadaraka baina ya boss na mfanyakazi mara nyingi humfanya mfanyakazi akose ujasiri wa kuongea pale boss wake anapokosea.

Ni vizuri kuongea ila zingatia hali ya boss wako ikoje ana furaha, huzuni au hasira ili uwe na uhakika ni wakati gani utamwambia pia tumia busara katika kuongea naye. Unapotaka kuanza kuongea fanya haya kwanza:

1. Jiulize kama itabadilisha chochote
Ili kuwa na hakika kama jambo utakalozungumza litaleta matokeo ni vyema kujiuliza je, boss wako anashaurika au kupokea maoni ya watu wengine?, Kama ni mtu wa kuamini katika mawazo yake tu na hasikilizi kutoka kwa wengine basi ni vyema usiongee chochote.

2. Weka hoja mezani
Usipeleke mawazo yako kama sheria bali tengeneza mazingira ya wewe na boss wako kujadiliana, na kama itawezekana mpe na mifano ya mambo aliyowahi kufanya kimakosa na ukayavumilia. Hii itasaidia kujua sehemu anazokosea na ikitokea akaanza kukufokea basi mwache aongee kwani inaweza ikawa njia yake ya kupunguza hasira.

                        > Mbinu 7 za kuishi na Boss mkorofi kazini

3. Tumia wawakilishi
Kutegema na uhusiano uliopo kati yako na boss wako utaamua kama uende moja kwa moja kuongea nae au utatumia mtu kwa ajili ya kwenda kuwasilisha hoja zako. Unaweza kumtumia Meneja rasilimali watu au hata msaidizi wa boss wako.

Migongano hutokea hivyo ni vizuri wote,  boss na mfanyakazi kutambua umuhimu wa kila mmoja kwa maendeleo ya kampuni au taasisi.

 

error: Content is protected !!