Tafiti: Sababu 4 za wanaume kujiua zaidi kuliko wanawake

HomeElimu

Tafiti: Sababu 4 za wanaume kujiua zaidi kuliko wanawake

Kila Novemba ni mwezi wa kuadhimisha afya ya akili kwa wanaume, takwimu kidunia zinaonesha wanaume wana uwezekano mkubwa wa kujitoa uhai kuliko wanawake.

Takwimu za Shirika la Afya duniani zinaonesha kuwa asilimia 40% ya mataifa yote duniani, katika vifo 100,000 vya kujitoa uhai basi 15 ni vya wanaume. Sasa ni kwanini wanaume hujitoa zaidi uhai kuliko wanawake?

1. Wanaume hawazungumzii hisia zao
Ni rahisi sana wa wasichana kuzungumza juu ya hisia zao aidha kwa rafiki au ndugu zao. Hii huwasaidia hasa kupunguza hisia za kutaka kujiua. Kuna msemo wa kizungu unasema “A problem told is a half solved” yaani, tatizo linapozungumzwa, basi ni nusu ya kupata suluhu ya tatizo hilo. Wanaume wanakaa sana na vitu moyoni pasi na kusema na kushirikisha mtu kuomba mawazo mbadala, hatua hii hupelekea wanaume wengi kujitoa uhai.

2. Uwezekano mkubwa wa kushiriki tabia hatarishi
Wanaume ndio watumizi wakubwa wa mihadarati pamoja na aina nyingine ya ulevi ukilinganishwa na wanawake. Utumiaji wa vilevi mara kwa mara hutuweka katika hatari zaidi ya kufanya maamuzi ya kutaka kujitoa uhai. Tabia ya ulevi hauthiri uwezo wetu wa kufanya maamuzi na kupelekea kufanya maamuzi ambayo sio mazuri kwa mustakabali wa maisha yetu.

3. Fedha zinaweza kumfanya mwanaume ajiue
Sehemu nyingi hapa duniani wanaume kazi yao kubwa ni kutumiza mahitaji ya kifamilia. Jukumu huchukuliwa kwa umakini mkubwa sana na wanaume. Wanaume wengi hukosa furaha pale wanaposhindwa kukidhi haja za msingi za watu wao wa karibu, hii ni tofauti sana na wanawake kwani jamii nyingi zimeshajengewa kuwa jukumu la mwanaume ni kutafuta pesa na watu wengine watumie. Hatua hii ikishindwa kufikiwa basi humpa mwanaume msongo na msukumo wa kufanya maamuzi ya kujitoa uhai wake.

4. Wanaume hawapendi kuonekana wameshindwa
Ushujaa ni sifa ya kila mwanaume, kila mwanaume anafurahi kuwa shujaa aidha kwa mtoto wake, mke wake au hata wazazi wake. Ushujaa huu huja na gharama zake pia, kufanya kazi kwa bidhii ili usidie wale unaotaka uwe shujaa wao. Hata kama watu wale wataona hali ya kushindwa kwako, pindi wakukuuliza ni aghalabu kukiri kuwa mambo sio mazuri, bali hutoa sababu za kuonesha kuwa unaendelea vizuri na utatimiza majukumu yako.

Gharama za kuwa mwanaume ni kubwa sana katika jamii zetu, misingi ya ugumuu hujengwa hasa na mila na desturi zetu ambazo kwa kiasi kikubwa zina mchango katika kupanga mitazamo yetu na namna ya kuchukulia mambo.

error: Content is protected !!