Hizi ni njia saba zitakazokusaidia kutunza fedha zako vizuri

HomeElimu

Hizi ni njia saba zitakazokusaidia kutunza fedha zako vizuri

Watu wengi wamekuwa na matumizi mabaya ya fedha zao kiasi cha kushindwa kufikia malengo yao kwa wakati unaopaswa.
Zifuatazo ni njia zinazoweza kutumika katika kusimamia fedha zako;

1. Tambua hali yako ya uchumi kwanza
Kabla hujaanza kupanga bajeti ya fedha zako hakikisha kwanza unajua hali yako ya kiuchumi.
Kujitathimi ulipo kiuchumi itakusaidia katika kupanga bajeti na matumizi ya fedha yako.

2. Weka vipaumbele
Ukishatambua ulipo, weka vipaumbele vyako utakavyoanza navyo katika matumizi ya fedha ili uhakikishe kwamba umetumia kwenye mambo sahihi, ili hata pale fedha itakapokwiisha unakuwa tayari umeshatimiza mambo ya msingi.

3. Andaa bajeti
Hakikisha unaanda bajeti ya matumizi ya pesa yako. Kwa kufanya hivi itakufanya uwe na nidhamu ya matumizi ya fedha kwani hutoweza kutumia kiasi kilicho nje ya bajeti yako uliyoiandaa.

4. Weka pembeni fedha ya dharura
Wakati unaanda bajeti yako hakikisha unaweka pembeni fedha ya dharura endapo itatokea ili usivuruge mambo uliyoyawekea vipaumbele.

5. Weka akiba ya kustaafu
Siku hizi sio kila kampuni inatoa mafao kama ukistaafu, hivyo ni vyema ukawa unajiwekea mafao yako pembeni. Mshahara unaopata chukua kidogo na tenga pembeni ili uweze kutumia baadae utakapostaafu.

6. Lipa madeni
Lipa madeni yako kwa wakati sasa ili uweze kuepuka riba kubwa.
Kuna baadhi ya mikopo ukichelewa kulipa basi riba yake inaongezeka, hivyo ili kuepuka na hali hii kwani itakua inakumalizia fedha zako ni bora ukawa unalipa madeni yako kwa wakati sahihi.

7. Tathimini matumizi yako ya siku
Hakikisha unatathimini matumizi yako ya kila siku, kwani kwakufanya hivi itakusaidia kutambua mwenendo wa matumizi yako ya fedha. Pia utajua kama upo ndani ya bajeti au nje ya bajeti.

error: Content is protected !!