Mtindo huu unaweza kusababisha uume kuvunjika wakati wa kujamiiana

HomeElimu

Mtindo huu unaweza kusababisha uume kuvunjika wakati wa kujamiiana

Tumezoea na tunafahamu kuwa mifupa ndiyo huvunjika, lakini pia ni mara chache kusikia uume unavunjika kama inavyotokea kwa mifupa pale inapopata hitilafu au ajali.

Kama ulikuwa hujui, basi uume nao unaweza kuvunjika na kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama “Penile Fracture”.

Katika hali ya kawaida uume unapokuwa umelala ni vigumu kuvunjika au kupata shida yoyote kwa sababu unakua mlaini na rahisi kujikunja. Pale uume unaposimama hapa ndipo shida inapoweza kutokea na ukiwa katika hali hiyo, uume iwapo utapindishwa au kukunjwa ghafla, tabaka lake la “tunica albuginea” ambalo liko kama mfuko linaweza kuchanika kwa takriban sentimita 0.5 hadi nne.

Kuvunjika kwa uume kunaweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi, kujichua (masturbation) na vyanzo vingine kama kupindishwa kwa lazima na kulala vibaya.

> Mbinu 3 rahisi za kutongoza mwanamke na kukubali bila vikwazo

Asilimia kubwa ya kuchanika kwa uume hutokea wakati wa kufanya mapenzi hasa pale mwenzi wa kike anapokuwa juu. Uzito wote unakua juu ya uume. Ikitokea uume ukateleza nje na kugonga mfupa wa nyonga ya juu (symphysis pubis) basi uzito wa mwenza utakuwa juu ya uume na kusababisha kuchanika.

Ni muhimu kuwa makini wakati wa kufanya mapenzi hasa uume unapokuwa umesimama ili kujilinda na hatari yoyote inayoweza kutokea. Hakikisha uume umeingia vyema katika uke na kwamba uke uwe umelainika vya kutosha.

Ikitokea zoezi limekua refu na uke bado mkavu, badilisheni mkao wa mapenzi. Na ikitokea uume umevunjika fika hospitali ufanyiwe upasuaji ambao ni tiba ya tatizo hilo.

error: Content is protected !!