Ghorofa la Samia larejesha wanafunzi shuleni

HomeKitaifa

Ghorofa la Samia larejesha wanafunzi shuleni

Shule ya Sekondari Ihanga jijini Mbeya ni kati za shule zilipewa fedha na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kujengwa kwa mfumo wa ghorofa kutokana na eneo lake kuwa finyu hivyo kutotosheleza ujenzi wa madarasa mengine ya chini.

Faraja Willa ambaye ni Afisa Mtendaji anaelezea hali iliyokuwepo kabla ya ujenzi wa ghorofa hilo na kusema kuwa litawasaidia wanafunzi na pia kuondoa hadha ya kuchangisha fedha wananchi za madarasa.

“Kama mimi ambaye ni Afisa Mtendaji moja kwa moja huwa tunakuwa tunachangisha michango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, huwa tunapata changamoto kubwa sana. Kwahiyo kiukweli mwaka jana nilikuwa nina waza hivi nitaanzaje na ukizingatia hili jengo ni la muda mrefu na watu wamechoka kuchanga michango. Kwa kweli alivyoziingiza hizo hela Oktoba 1, 2021 binafsi nilifurahi sana,” alisema Faraja.

Ghorofa jipya la Shule ya Sekondari Ihanga, Mbeya.

Naye mwanafunzi Lulu Andende ameeleza kufurahishwa na ujenzi wa ghorofa hilo huku akisema sasa hali itakuwa tofauti na zamani kwani walikuwa wakilundika wanafunzi wengi darasani na wnegine kukaa chini.

“Wakati naanza kidato cha kwanza tulikuwa wanafunzi wengi sana ambapo ilibidi darasa moja tukae wanafunzi zaidi ya 50, baadhi ya wazazi kutokana na ile hali wanafunzi wengi wanakaa darasa moja wakaamua kuwatoa watoto wao katika hii shule. Lakini sasa tumejengewa hili ghorofa na madarasa yapo yakutosha,” alisema Lulu.

 

 

 

 

error: Content is protected !!