Leo katika Historia: Dakta Fathi Shiqaqi, Katibu Mkuu wa Jihadi ya Islami anauawa

HomeElimu

Leo katika Historia: Dakta Fathi Shiqaqi, Katibu Mkuu wa Jihadi ya Islami anauawa

Tarehe kama ya leo mwaka 1995 afisa wa shirika la ujasusi la Israel Mossad walifanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina, Dkt. Fathi Shiqaqi, akiwa huko Malta.

Shiqaqi alizaliwa mwaka 1951 katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza. Alihitimu masomo ya udaktari na kufanya kazi katika hospitali moja ya Baitul Muqaddas. Alianzisha harakati za mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel akiwa kijana.

Mwaka 1979 Shiqaqi alikamatwa na kusweka jela nchini Misri kwa sababu ya kuandika kitabu kuhusu harakati za Imam Ruhullah Khomeini na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Aliitangaza Siku ya Kimataifa ya Quds iliyoainishwa na Imam Khomeini, kuwa ni siku ya kuhuisha uislamu na mapambano ya jihadi dhidi ya Wazayuni huko Palestina.

error: Content is protected !!