Familia yakataa kumzika ndugu yao aliyeua watoto 10

HomeKimataifa

Familia yakataa kumzika ndugu yao aliyeua watoto 10

Familia ya mshukiwa sugu wa mauaji ya watoto zaidi 10 aliyeuawa kwao baada ya kutoroka mahabusu ya polisi imemkana na kusema haitomzika kwa sababu inahofia kupata laana kutokana na kile alichokifanya ndugu yao huyo aliyefahamika kwa jina la Masten Wanjala (20).

Naibu Chifu wa Mukhweya, Abiud Musungu, alisema kuwa familia ya Wanjala ilikataa kupokea simu kutoka kwa maofisa ili wachukuliwe vipimo vya vinasaba -DNA na kumzia kijana huyo. huku akisema serikali huenda ikalazimika kumzika mshukiwa huyo wa mauaji iwapo familia itaendelea kuwa na msimamo wa kumkana.

Jirani wa Wanjala, Davis Wafula alisema kuwa kama ukoo hawakutaka kujihusisha naye kwa sababu aliwaaibisha na hivyo wanaogopa kuonekana kama wauaji.

Kabla ya kifo chake Masten Wanjala alikiri binafsi kuwaua watoto zaidi ya 10 katika kipindi cha miaka mitano na wakati mwingine kunywa damu zao.

error: Content is protected !!