Shilole: Kiba, Nasibu humuwezi tusikudanganye

HomeBurudani

Shilole: Kiba, Nasibu humuwezi tusikudanganye

 

Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha clouds FM msanii Ali Kiba, amesema kwamba hakumualika Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘Only One King’ aliyoizindua mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

“Kama kuna mtu ana bifu naye alialikwa mimi sikumwalika huyo mtu. Sikumwalika Shilole nilistukia tu yupo pale ukumbini na nisingeweza kumkumbuka Shilole kwa sababu sina mazoea naye. Esha namkumbuka sana. Hata unilazimishe vipi nisingeweza kumkumbuka Shilole hatupo karibu kabisa,” alisema Kiba.

Baada ya maneno hayo kutoka kwa Ali Kiba, Shilole aliamua kuvunja ukimya na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba hana utu kama jinsi watu wengi wanavyosema kuwa Kiba hamuwezi Nasibu akimaanisha Diamond Platnumz.

“Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu, utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu? Kwa hiyo hata Nasibu uliyeshindana naye miaka mingi akakugaragaza angeweza kualikwa bila wewe kujua? (Nasibu humuwezi tusikudanganye). Wewe ndo msanii wetu wa kimataifa? SIJAPENDA,” ameandika Shilole.

Shilole ameonyesha kuchukizwa na jambo hili kwani Ali Kiba alipost picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimuomba awepo kwenye shughuli yake hile ya uzinduzi wa albamu.

error: Content is protected !!