Baba Levo: SGR kuibadilisha Kigoma kiuchumi

HomeKitaifa

Baba Levo: SGR kuibadilisha Kigoma kiuchumi

Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma ni mradi wa kimkakati utakaobadilisha uchumi wa mkoa huo na kuboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa reli hiyo, Baba Levo amesema wananchi wa Kigoma wameusubiri kwa muda mrefu mradi huo na wanaamini utarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo, pamoja na kuongeza fursa za biashara na uwekezaji.

Amesema kukamilika kwa reli hiyo kutaiunganisha Kigoma kwa ufanisi zaidi na maeneo mengine ya nchi, hatua itakayochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kuifanya Kigoma kuwa kitovu muhimu cha biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Mbunge huyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, akisisitiza kuwa wananchi wa Kigoma wataendelea kushirikiana kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

error: Content is protected !!