SGR Tabora-Kigoma kufungua fursa mpya za kiuchumi

HomeKitaifa

SGR Tabora-Kigoma kufungua fursa mpya za kiuchumi

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa Taifa kwa kufungua fursa mpya za uwekezaji, biashara na maendeleo ya viwanda katika ukanda wa magharibi mwa Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi huo, Rais Samia amesema Serikali imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya reli na barabara ili kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo, kupunguza gharama za usafiri na kuongeza ushindani wa Tanzania katika biashara za kikanda na kimataifa.

Amesema kukamilika kwa reli hiyo kutachochea ukuaji wa miji iliyopo kandokando ya njia ya reli, kuongeza shughuli za kiuchumi na kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, biashara, madini na kilimo.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati inaendelea kutekelezwa kwa wakati ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia fursa zinazozalishwa na uwekezaji wa Serikali, akisisitiza kuwa SGR ni nguzo muhimu ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

error: Content is protected !!