Salim Kikeke aaga BBC

HomeKitaifa

Salim Kikeke aaga BBC

Mtangazaji nguli wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) ,Salim Kikeke ametangaza kustaafu kazi katika shirika hilo baada ya kulitumikia kwa miaka mingi.

Kikeke ambaye ni Mtanzania ameaga rasmi jana Aprili 28,2023 wakati akihitimisha Dira ya Dubia na kusema kuwa anakwenda kufanya majukumu mengine lakini hajaweka wazi anakwenda wapi.

“Nimekuwa na wakati mzuri hapa Londo tangu nilipojiunga na BBC nikiwa redio, kisha televisheni, ninakwenda kufanya majukumu mengine na leo hii itakuwa mara yangu ya mwisho kutangaza Dira ya Dunia.

“Ninawashukuru wafanyakazi niliokuwa nikifanya nao kazi hapa BBC na vyombo vingine vya habari nilivyofanya nao kazi kabla sijaja hapa, wote mmenisaidia sana kutimiza ndoto zangu na kunifikisha nilipo.” alisema Kikeke.

error: Content is protected !!