Rais Samia : Mchengerwa ni bingwa wa mabadiliko

HomeKitaifa

Rais Samia : Mchengerwa ni bingwa wa mabadiliko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Waziri mpya wa OR- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kuleta mabadiliko kwenye kila sekta aliyohudumu.

Amesema hayo alipokuwa akiwaapisha viongozi wateule Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo tarehe 01 Septemba, 2023.

“Kwa mfano Mchengerwa nilipompeleka utumishi mwanzo kaingia na kasi kelele zikawa nyingi, nikasema labda waziri wangu kazidi kapandisha mabega nimpeleke michezo, kaenda michezo kazi aliyoifanya mmeiona, kaacha kazi nzuri sana, katoka michezo nimempeleka utalii, mipango aliyoiweka sekta ile unayeenda ukienda ukafuata yaliyowekwa utalii unakwenda kupanda”amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amemtaka Waziri Mchengerwa kwenda kuendeleza uchapaji kazi kwenye wizara yake ya sasa ya TAMISEMI na kufanya mabadiliko kama kwenye sekta alizopita.

“Sasa Mchengerwa nimempeleka TAMISEMI, mwakani kuna kivumbi na mimi nakujua najua unaweza, kivumbi kile kinafanana na kifua chako najua unaweza, kwahiyo nimekupeleka TAMISEMI ni kazi kazi, sasa mengine sitaki kuyachambua hapa wanasema usimwage mtama kwenye ndege wengi”amesema.

error: Content is protected !!