Rais Samia Suluhu mfanyakazi bora

HomeKitaifa

Rais Samia Suluhu mfanyakazi bora

Wakati leo ni sikukuu ya Wafanyakazi duniani, Umoja wa Wanawake Wanasiasa Tanzania (ULINGO), umempatia Tuzo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kuwa mfanyakazi bora mwaka huu.

Tuzo hiyo imetolewa kutokana na uwakilishi wake mzuri alioonesha katika kuongoza nchi kwa miaka miwili, huku akifuata Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Akipokea tuzo hiyo jijini Dar es Salaam, jana kwa niaba ya Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama alisema Rais Samia ana haki zote za kupewa tuzo kutokana na kutimiza vizuri majukumu yake na ameonesha uwezo mkubwa ndani ya kipindi cha miaka miwili madarakani.

error: Content is protected !!