Rais Samia: tuwaenzi waasisi wetu kwa vitendo

HomeKitaifa

Rais Samia: tuwaenzi waasisi wetu kwa vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania wote kuenzi kwa vitendo muungano ulioanzishwa na waasisi wa taifa letu.

Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Muungano na Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais , Rais Samia amesema kwa kuwaenzi waasisi wetu tunapaswa kufanya kazi kwa bidii na kudumisha amani.

“Niwasihi watanzania wote kuendelea kudumisha amani na mshikamano wa taifa letu, kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kudumisha uzalendo kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wetu wa Muungano.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewasihi watanzania kusoma vitabu hivyo ili waweze kujiongezea maarifa zaidi na kufahamu historia ya taifa letu.

error: Content is protected !!