Rais Samia awakaribisha Waturuki kuwekeza nchini

HomeKitaifa

Rais Samia awakaribisha Waturuki kuwekeza nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Uturuki kuwekeza nchini Tanzania na kuwaahidi ushirikiano.

Amesema hayo leo Aprili 19,2024 alipokuwa akihutubia katika Jukwaa la wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki jijini Istanbul na kuwaomba kushirikiana wakati huu ambao Tanzania ipo kwenye safari ya mabadiliko ya kiuchumi.

“Ninawaalika kwa dhati Waturuki kuwekeza Tanzania. Tanzania inahitaji msaada wa kimataifa katika safari yake ya mabadiliko ya kiuchumi. Ombi langu kwa marafiki zangu wa Kituruki ni kwamba tuanze safari hii pamoja,” amesema Rais Samia.

Akihutubia jukwaa hilo, Rais Samia amesema biashara kati ya Tanzania na Uturuki inapaswa kufunuliwa na kukua zaidi huku akisisitiza kwamba Tanzania ipo katika eneo zuri la kijiografia hivyo ni rahisi kwa Uturuki kuwekeza nchini.

 

error: Content is protected !!