Utalipwa Milioni 3 kutazama filamu za kutisha

HomeKimataifa

Utalipwa Milioni 3 kutazama filamu za kutisha

Inaonekana kuwa kazi ngumu na ya kutisha, lakini ni njia rahisi pia kuingiza fedha.

Kampuni ya FinanceBuzz huko nchini Marekani inatafuta mtu ambaye ataweza kutazama filamu 13 za kutisha ambazo hazijawahi kutazamwa popote.Mtu atayefanikiwa kupata kazi hiyo, atalazimika kuvaa kifaa maalumu mkononi mwake wakati wote akitazama filamu zote 13.

Lengo la kifaa hicho ni kufuatilia mapigo ya moyo ya mtazamaji wakati wa kutazama filamu hizo.Wakati kampuni hiyo inaongea na vyombo vya habari, wamesema kuwa lengo la utafiti huo ni kutazama kwamba gharama/bajeti, ndogo au kubwa, ila athari yoyote kwa mtazamaji hasa kwenye filamu za kutisha.Kampuni ilitangaza kwamba inahitaji  mzoefu wa kutazama filamu zote 13.

Lengo ni kuangalia je, filamu za kutisha zenye gharama kubwa ndio zinazotisha zaidi kuliko filamu za kutisha za gharama ndogo?

Majibu ya utafiti huu yatawezesha kujua bajeti kiasi gani iwekwe kwenye kutengeneza filamu za kutisha. Mtazamaji picha atahitajika kukisia kiasi cha bajeti kilichotumika kwenye kila filamu kulingana na uzoefu wake. Maombi ya kazi hiyo yataanza tarehe 26 Septemba na mshindi kutangazwa mwezi Oktoba

error: Content is protected !!