TikTok kuanza kutumika kwenye “Smart TV”

HomeBurudani

TikTok kuanza kutumika kwenye “Smart TV”

Mtandao wa TikTok ambao umekuwa jukwaa la elimu na burudani unaingia katika vitabu vya historia kati ya mitandao ya kijamii yenye ‘app’ ya moja kwa moja kwenye televisheni hivyo kuwapa watumiaji wake uwanda mpana wa matumizi.

Mtandao wa kijamii wa TikTok ambao unaruhusu mtu kupakia maudhui ya video za hadi dakika tatu umezindua programu tumishi (app) ambayo itaanza kutumika kwenye televisheni janja za kampuni ya LG hivi karibuni.

Televisheni za LG ambazo zitafikiwa na TikTok ni za matoleo ya kuanzia mwaka 2019. Hata hivyo “app” ya Tiktok imetengenezwa kutumika kwenye simu (portrait mode) hivyo upana wa televisheni unaweza usiwe na muonekano mzuri kwa mtumiaji.

Imeelezwa kuwa baada ya app hii kuanza kutumika, TikTok itakuwa inajitegemea kama zilivyo apps za YouTube, Netflix na Prime Video kwenye televisheni janja (Smart TV)

error: Content is protected !!