Sababu za kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

HomeElimu

Sababu za kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

Zifuatazo ni sababu za kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

1.Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.

2.Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu makali katika shingo ya kizazi inapogusana na uume.

3.Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.

    > Mambo 7 ya kushangaza usiyoyajua kuhusu tendo la ndoa

4.Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.

5.Kuumia uke: majeraha kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.

6.Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.

error: Content is protected !!