Mambo 7 ya kushangaza usiyoyajua kuhusu tendo la ndoa

HomeElimu

Mambo 7 ya kushangaza usiyoyajua kuhusu tendo la ndoa

Tendo la ndoa huaminika kuwa miongoni mwa mambo ya kale zaidi ulimwenguni na bila shaka, binadamu wasingeendelea kuwepo bila kuendelea kufanyika kwa tendo hili. Hapa tunaangazia ni kwa jinsi jamii mbalimbali zinavyoshiriki katika tendo hili pamoja na imani zinazohusiana na tendo hili zilivyo tofauti kutoka eneo moja hadi jingine duniani.

1.Colombia wanaume hupigwa ngwara
Katika jamii ya Guajiro, mwanamke hujipatia mwanaume wa kumuoa baada ya kumpiga ngwara na kumwangusha wakati wa kucheza ngoma za kitamaduni. Kutokuwa na nguvu bila shaka kwa wanaume hawa ni nafuu. Iwapo mwanamke atafanikiwa kumwangusha mwanaume kwa kumpiga ngwara, basi wawili hao ni lazima washiriki tendo la ndoa.

2.Wagiriki ndio hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya kondomu za Durex, ambao ulishirikisha watu takribani 30,000 wenye umri wa miaka zaidi ya 16 kutoka mataifa 26. Wagiriki wanaongoza kwa kushiriki tendo la ndoa. Kwa wastani, Wagiriki hufanya tendo la ndoa mara 164 kwa mwaka.

Hali ya hewa nchini Ugiriki, ambapo hakuna baridi sana au joto linalopita kiasi, pamoja na uwepo wa bustani nzuri za mizeituni, zinatajwa kama sababu zinazochochea hili. Hata katika filamu ambazo huonesha utamaduni wa Wagiriki, suala la wao kuonekana kama jamii ya watu wanaopenda kushiriki tendo la ndoa huonekana wazi.

3. Korea Kusini Wanawake hawataki kupata Watoto
Kwa wastani, mwanamke nchini Korea Kusini anakadiriwa kupata mtoto mmoja pekee maishani mwake. Lakini Taifa hilo linahitaji kiwango cha watoto angalau 2 kwa kila mwanamke ili kudumisha uthabiti katika idadi ya watu nchini humo. Kiwango hiki ni maradufu ya kiwango cha sasa. Ili kujaribu kutatua shida hiyo, serikali imewekeza mabilioni ya fedha katika kampeni ya kuwahamasisha wanawake kuzaa, lakini kiwango kimeendelea kushuka.
Huenda ikawa inatokana na kupanda kwa gharama ya maisha na gharama ya kuwalea watoto, lakini pia huenda inatokana na muda mrefu ambao watu hufanya kazi kwa siku nchini humo.

> Sababu sita zinazoweza kumfanya mwanamke achepuke

4. Denmark ni mabingwa wa kubebesha mimba wakiwa likizo
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni moja ya safari za kitalii, raia wa Denmark hushiriki tendo la ndoa kwa wastani asilimia 46 zaidi wakiwa likizo na katika safari za kitalii. Asilimia 10 ya watoto wote Denmark mimba zao hupatikana wazazi wao wakiwa likizo ama safari za kitalii. Mwaka 2014, kampuni ya Spies Travel iliahidi zawadi ya mahitaji kwa mtoto wa miaka mitatu pamoja na likizo murua kwa wanandoa ambao wangethibitisha kwamba mimba ya mtoto wao ilitungwa wakiwa katika safari iliyopangwa na kampuni hiyo.

5. Urusi kuna siku ya Kutungwa kwa Mimba
Jimbo moja nchini Urusi limeanzisha njia ya kipekee ya kusaidia watu kuzaliana kwa wingi baada ya kugundua kwamba idadi ya watu inapungua kwa kasi. Gavana wa jimbo la Ulyanovsk, mashariki mwa Moscow alitangaza tarehe 12 Septemba kila mwaka kuwa Siku ya kubebesha mimba. Hii ni siku ya mapumziko ambapo wanandoa huhamasishwa kukaa nyumbani kwa lengo moja pekee, kuhakikisha mimba inatungwa na watoto kuzaliwa. Wanandoa wanaojaliwa watoto miezi 9 baada ya siku hiyo hupewa zawadi nono.

6. Australia wanawake huweka matufaa kwenye makwapa
Ni utamaduni wa miaka mingi kwa maeneo ya mashambani nchini Australia, wanawake kupasua matufaha, kuyaweka kwenye makwapa yao na kisha kuwapa wanaume wanaowachumbia wakati wa ngoma ya kitamaduni.
Iwapo mwanaume atalifurahia tufaa hilo baada ya kulinusia ni jibu tosha kuwa anampenda mwanamke huyo na hilo hudhihirishwa kwa mwanaume kumega kipande cha tufaa hilo lililojawa na jasho.

7. Wajapani hawashiriki tendo la ndoa sana
Japan ni taifa jingine ambalo linashuhudia kushuka kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa. Matumizi ya kondomu, tembe za kuzuia kushika mimba na visa vya maambukizi ya magonjwa ya zinaa vyote vinashuka. Kunio Kitamura, ambaye ni mkuu wa chama cha uzazi wa mpango nchini Japan anasema, “Ufafanuzi pekee wa kueleza hili ni kwamba Wajapani wameanza kupunguza ushiriki wao wa tendo la ndoa.”

Ripoti ya hivi majuzi ilibaini kwamba idadi ya wanandoa ambao wanaishi pamoja bila kushiriki tendo la ndoa imeongezeka sana. Theluthi moja ya wanaume walisema huwa wanachoka sana kiasi cha kutokuwa na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

error: Content is protected !!