SIMBA: Kila la heri Morrison

HomeMichezo

SIMBA: Kila la heri Morrison

Taarifa kwa Umma kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba iliyowekwa kwenye ukurasa wa klabu hiyo ya twitter inasema kwamba;

Klabu ya Simba imempa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji wake Bernard Morrison.

Simba imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.

Simba inamshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu hiyo yetu.

Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klbau yetu na kuisaidia kupata mafanikio kadhaa ikiwemo kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kwa mchango na mafanikio hayo klabu inashukuru mchezaji huyo kipenzi cha wanasimba kwa kujitoa kwake kuipigania klabu yake.

Simba inamtaki kila la heri Bernard Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadae.

 

error: Content is protected !!