Nchimbi akubali yaishe, ajiengua Yanga

HomeMichezo

Nchimbi akubali yaishe, ajiengua Yanga

Wakati kikosi cha wana Jangwani Yanga kilikuwa visiwani Zanzibar kikiendelea na maandalizi ya Ligi, mshambuliaji wao Ditram Nchimbi amejiondoa mwenyewe kikosini.

Nchimbi alijiunga na Yanga Desemba 19 2019 ameitumikia timu hiyo miaka miwili baada, baada ya kuona mambo hayajaenda kama yalivyotarajiwa ameamua mwenyewe kujiondoa kwenye kikosi cha wana hao wa Jangwani.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amelithibitisha kuwa ni kweli mchezaji huyo hayupo pamoja na timu ni baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi haujaonyesha nia ya kumuongeza mkataba.

“Mkataba wake umeshakwisha na mchezaji mwingine ambaye mkataba wake upo ukingoni ni Adeyum Saleh yeye anamalizia msimu huu sijajua kama uongozi utakuwa na mpango naye,” alisema.

Alisema Ditram ameshaaga hatakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga akizungumzia maandalizi yao kwa ujumla alisema wanaenda vizuri na mipango ya kocha imeenda kama ilivyopangwa. “Kocha aliomba michezo miwili yote imechezwa wachezaji wote ameona mapungufu na uwezo wao hasa nyota ambao walikuwa nje kwa muda mrefu kama Yasin Mustafa amerudi na amepewa muda wa kucheza sasa ni yeye kuamua.”

error: Content is protected !!