Penzi la Kigosi, vita kali Johari na Chuchu

HomeBurudani

Penzi la Kigosi, vita kali Johari na Chuchu

Waigizaji kutoka Tanzania Blandina Chagula maarufu kama “Johari” na mwanadada Chuchu Hans ni kama wameingia kwenye mvutano uliopelekea kurushiana maneno katika mtandao wa kijamii wa Instagram huku ukihisiwa kuhusishwa na kumgombania muigizaji mwenzao Vincent Kigosi maarufu kama Ray.

Kabla ya Chuchu Hans kuanza mahusiano na Ray yaliopelekea kupata mtoto wa kiume, zamani wakati filamu za kibongo zimeshika kasi ilidaiwa kuwa Ray na Johari wamo kwenye mahusiano na baadae walikuja kufungua kampuni yao ya pamoja ya kutengeneza filamu iliokua inajulikana kama RJ lakini kampuni iyo ilivunjika kwa sababu wanazozijua wao wenyewe na kila mmoja anafanya kazi zake kwa sasa.

Ugomvi wa Chuchu na Johari ni kama kuna sehemu ulianzia, ukaja kumalizikia Instagram katika ukurasa wake wa Instagram ambapo Johari alisema, “Nawatizama na kuwadharau maana kinyago nilichochonga mwenyewe kamwe hakiwezi kunitisha” .

Chuchu Hans pia aliweka jumbe mbili mmoja ulikuwa unaosomeka “Ukiona umeshinda tambua sijaamua kushindana na wewe, na ukiona ameniacha ujue nimeamua mwenyewe kinyago kisichokutisha umekosea kukichonga” na ujumbe mwingine aliouweka ulikua unasomeka “Sio kila bibi kizee ana busara maana kuna wajinga pia wamezeeka hivyo ukimya wao ni faida kwako maana wakiongea maneno yao hayana faida kwako”.

error: Content is protected !!