Sekta ya madini yafikia lengo la mchango wake kwenye Pato la Taifa

HomeKitaifa

Sekta ya madini yafikia lengo la mchango wake kwenye Pato la Taifa

Serikali imesema mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umefikia asilimia 10.1.

Taarifa hiyo imetolewa jana Dodoma na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akieleza mafanikio katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

“Mwaka 2023 tulikuwa na mchango wa asilimia 9.1 kwenye Pato la Taifa. Leo hii tunazungumza kuhusu ongezeko hadi asilimia 10.1 kwa mwaka 2024. Hili si jambo dogo,” alisema Mavunde.

Waziri Mavunde alisema mafanikio hayo yametokana na mabadiliko ya kimfumo na kisheria yaliyofanyika katika sekta ya madini tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Sita.

Miongoni mwaka hatua zilizochangia mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia sekta hiyo, kuanzishwa kwa minada ya madini ya vito, udhibiti wa utoroshaji wa madini, kuanzishwa kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini na kuanza kwa ununuzi wa dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

error: Content is protected !!