Askari auawa kwa mshale Ngorongoro

HomeKitaifa

Askari auawa kwa mshale Ngorongoro

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amewataka wananchi Wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro Kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.

Mongella  ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amesema hayo leo June 11 2022 katika tarafa ya loliondo wilaya ya Ngorongoro  alipokuwa anaongea na vyombo vya habari kuhusiana na zoezi linaloendea la uwekaji mipaka katika wilaya hiyo.

Amewambia waandishi wa habari  kuwa kuna baadhi ya watu na mitaandao ya kijamii kupotosha kuhusiana na kinachoendelea katika zoezi la uwekaji mipaka katika wilaya ya Ngorongoro.

Kutokana na picha na video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha watu wamejeruhiwa huku wakihusisha na zoezi hilo la uhamishwaji wa wakazi wa Ngorongoro, Mongella amesema kama kuna aliyejeruhiwa na mamlaka ajitokeze kwa sababu mpaka sasa hawajapokea mtu yoyote hospitali.

“Kama kuna mtu yoyote anajeraha kutokana na chochote ambacho anadhani kimesababishwa na vyombo vyetu au mamlaka zetu basi ajitokeze ili aweze kupata huduma,”amesema Mongella.

Aidha amesema kuwa katika siku ya jana kulitokea kundi la watu wenye silaha  ambapo askari wetu alijeruhiwa na kukimbizwa hosptali lakini alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu.

 

error: Content is protected !!